Habari za Mastaa

Lady Gaga aamua kuufuta wimbo alioshirikiana na R Kelly

on

Fahamu kuwa Muimbaji wa Pop Lady Gaga ameahidi kuifuta kolabo aliyowahi kuifanya na R Kelly mwaka 2013 ‘Do What You Want’ kutokana na nguli huyo kuandamwa na tuhuma ya unyanyasaji wa ngono kwa wanawake.

Lady Gaga ameahidi kufuta wimbo huo kwenye mitandao ya kusikiliza na kupakua nyimbo mtandaoni na pia ameomba radhi kwa kuwahi kufanya kazi na R Kelly. Filamu ya Surviving R Kelly imepata mtazamo hasi baada ya wanawake tofautitofauti kutoa ushuhuda.

Chance The Rapper akiwa miongoni mwa wasanii waliochukizwa na tuhuma za R Kelly alitoa taarifa kuwa anajutia kuwahi kufanya kazi na nguli huyo.

UWOYA KAWAFUNGUKIA NI KUHUSU KUWA NA WANAUME WENGI & NYUMBA

Soma na hizi

Tupia Comments