AyoTV

Kama uliwaogopa majaji wa BSS hii ndio zamu yako kutusua

on

Good News kwa vijana wa kitanzania ambao wamekuwa na malengo ya kupata nafasi za kuonesha vipaji vyao vya kuimba, baadhi ya vijana wamekuwa wakikosa ujasiri wa kusimama na kuimba mbele ya majaji licha ya kuwa na vipaji vikubwa.

Leo Chief Jaji wa Bongo Star Search Ritha Poulsen ameongea na waandishi wa habari na kuweka wazi namna ya vijana waliokosa nafasi ya kuonesha uwezo wao wa kuimba mbele ya majaji kwa hofu au kutokana na kukosa nauli ya kwenda mikoa ya jirani kufanya Audition.

Taarifa ikufikie kuwa leo Madam Ritha ametangaza kuwa mwaka huu kwa mara ya kwanza BSS itakuwa na Online Aution, yaani mshiriki atapata nafasi ya kurekodi video yake ya dakika moja na kuipost katika instagram yake huku akiweka hashtag maalum na majaji watachagua mshindi mmoja atakayeungana na washiriki wengine 16 wa BSS msimu wa 9.

BONYEZA PLAY KUTAZAMA NAMNA YA KUSHIRIKI BSS ONLINE AUDITION

Vimbwanga vya Papa Mafidoo vinaendelea “Mimi ndo CEO wa BSS”, amtaja Wema, Hamisa

Soma na hizi

Tupia Comments