Habari za Mastaa

PICHA: Ay leo katuonyesha Mke wake mtarajiwa kwa mara ya kwanza

on

Labda tutaona Harusi au ndoa ikifungwa siku zijazo? hilo ni swali tunaweza kubaki nalo lakini kwa sasa cha kufahamu ni kwamba Instagram leo ni ya Ay, miongoni mwa Wasanii wa longtime kwenye bongofleva.

Ambwene Yessaya hajawahi kumpost Shemeji yetu kwenye mitandao ya kijamii lakini amevunja ukimya na  kuichangamsha Instagram leo baada ya kumpost Mrembo anaeaminika kuwa wa kwake na maneno yanayosema ‘Heri ya siku ya kuzaliwa kwa mke wangu mtarajiwa, NAKUPENDA SANA na unajua#Kibokoyangu

Kwenye post ya pili Ay ambaye kwa mujibu wa mtandao kwa sasa ana umri wa miaka 35 akiwa amezaliwa July 5 1981, aliandika ‘A Trip down memory lane #MaliyaZee #ZeeMapenziniLEO’

screen-shot-2016-12-27-at-2-27-18-pm

screen-shot-2016-12-27-at-2-27-37-pm

VIDEO: Tazama Vodacom Wasafi Beach Party 2016 ilivyofana, Diamond, Vera Sidika na wengine kwenye hii video hapa chini

VIDEO: Kitu Diamond Platnumz amefanya Vodacom Wasafi Festival Iringa tazama kwenye hii video hapa chini

Soma na hizi

Tupia Comments