Premier Bet

AyoTV

VIDEO: “Hakuna mtu atapata uongozi CCM kama hajapita pale” – Humphrey Polepole

on

Katika kuhakikisha kinajiimarisha zaidi Chama cha Mapinduzi ‘CCM’ kinatarajia kujenga Chuo cha Uongozi kwa ajili ya wanachama wake na watanzania ambao watatakiwa kusoma chuoni hapo kama wanataka kuwa viongozi kupitia chama hicho.

Akizungumza leo April 30, 2017 katika Mahafali ya Umoja wa CCM Vyuo Vikuu Arusha, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole amesema kuwa chama kitajenga Chuo cha uongozi na hapatokuwa na kiongozi wa chama na serikali kupitia chama hicho ambaye atapatikana bila kusoma Chuo hicho.

“Hiki Chuo kitafundisha wana CCM. Hakuna mtu atapata uongozi kwenye Chama Cha Mapinduzi kama hajapita pale. Hakuna mtu atapata uongozi kwenye serikali kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi kama hajapita pale.” – Humphrey Polepole.

AyoTV MAGAZETI: Janga jipya kwa wenye vyeti feki, Kanisa lavunjwa, majoho yachomwa moto. Bonyeza play kutazama…

Soma na hizi

Tupia Comments