DSTV

Tangaza Hapa Ad

Michezo

MAAJABU: Chile ilianza game vs Brazil ikiwa ya tatu, ikamaliza nafasi ya 6

on

STAA wa FC Barcelona Lionel Messi alifunga hat-trick na kuisaidia Argentina kutoka nyuma kwa bao 1-0 na kushinda mabao 3-1 ugenini dhidi ya Ecuador na kujihakikishia kucheza fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.

Kwa matokeo hayo, Argentina imemaliza katika nafasi ya tatu kutoka nafasi ya sita ambapo walikuwa katika hatari ya kuzikosa Fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1970.

Kwingineko katika michezo mingine ya kufuzu fainali hizo kwa upande wa Amerika ya Kusini, Brazil ambayo ilishafuzu ilijihakikishia uongozi kwenye Kundi baada ya kushinda mabao 3-0 dhidi ya Chile ambayo yenyewe inamaliza katika nafasi ya sita licha ya kuingia katika mchezo huo wakiwa nafasi ya tatu. Mabao ya Brazil yakifungwa na Paulinho na Gabriel Jesus aliyefunga mara mbili.

Luis Suarez alifunga mara mbili Uruguay ikiichapa Bolivia mabao 4-2 kufuzu, huku Colombia ikisonga mbele baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Peru ambayo inamaliza katika nafasi tano kutoka Amerika ya Kusini na italazimika kucheza na New Zealand kwenye mchezo wa mtoano.

List ya majina 30 ya wanaowania tuzo ya Ballon d’Or 2017

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement