Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Kingine usichokijua kuhusu Rapa Colonel Mustapha kutoka Kenya

on

Kutoka 254 Kenya leo nimeipata hii stori kuhusu Rapa aliyewahi member wa kundi la The Vultures, Mustapha Colonel ambaye aliwahi kuingia kwenye headlines mara kadhaa baada ya kujitangaza kuwa anatoka kimapenzi na Female Star Huddah Monroe kutoka Kenya.

Nakuletea mambo matano ambayo huenda ulikuwa hujui kuhusu rapa Colonel Mustapha.

1. Rapa huyu alimpata mpenzi wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 20, baada ya kumaliza high school.

2. Busu la kwanza alilifanya na binamu yake. Binamu yake Mustapha alimfundisha rapa huyo jinsi ya kukiss ili amuunganishe na rafiki yake ambaye alikua akitaka kudate naye.

3. Zawadi yake ya kwanza ya Valentine’s Day ilikua ni box ya Condoms alizopewa na baba yake mzazi.

4. Kodi yake ya kwanza  ya nyumba ilikua Shilingi elfu nane (8,000) za Kenya ambazo ni sawa na Shilingi laki moja na sabini na mbili za Tanzania (172,902).

5. Gari ya kwanza kuiendesha ilikua Toyota Rav 4 na ilikuwa ya rafiki yake.

Rapa huyo kutoka Kenya pia ametangaza kuwa yuko kwenye harakati za kuoa hivi karibuni. Colonel Mustapha amesema kuwa amekamilisha process za awali na kilichobaki ni kwenda kulipa mahari kwenye familia ya girlfriend wake aitwaye Mikato.

>>>Tumekuwa pamoja kwa muda wa miaka miwili mpaka sasa, na nimegundua kuwa niko tayari kupeleka ng’ombe 50 kwenye familia yao ili nimchukue moja kwa moja:- Colonel Mustapha

Ikumbukwe kabla ya kukutana na Mikato, Mustapha aliwahi kudate na mastaa wengine wakubwa nchini Kenya akiwemo msanii wa muziki wa Genge, Marya pamoja na Huddah Monroe, ambaye ilikuja kubainika kuwa ilikua ni Public Stunt.

Nakusogezea picha 5 Colonel Mustapha akiwa na mpenzi wake mpya anayetarajia kumuoa hivi karibuni.

musta

mus2

mus1

mus4

mus3

ULIMISS KUONA CHUMBA CHA HOTEL ALIYOLALA CHRIS BROWN MOMBASA KENYA? NIMEKUWEKEA HAPA

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement