Tangaza Hapa Ad

Mix

DC Kigamboni kaongea, sababu 2 zilizofanya aagize Waalimu washushwe vyeo

on

Matokeo ya mtihani wa FORM IV kwama 2016 yametoka na miongoni mwa Shule 10 zenye Wanafunzi waliofeli zaidi Tanzania, 6 zinatoka Dar es salaam na hiyo imemfanya Mkuu wa wilaya ya kigamboni Hashim Mgandilwa kufanya uchunguzi kwenye hizo shule.

Baada ya uchunguzi wake Mkuu huyu wa wilaya ameagiza kushushwa vyeo kwa Wakuu wa shule mbili za za Sekondari ambazo ni Kidete na Somangila Day na amesisitiza ‘Ni kweli nimefanya hivyo na kuna sababu kubwa mbili’

Sababu ya kwanza ni kufelisha na pili kuna mmoja amepata ukuu wa shule katika namna ambayo ina ukakasi na inaonekana kwa namna moja ama nyingine kuna Watu walimtengenezea kukipata hicho cheo

Hiyo ilileta mvutano shuleni na baadhi ya Walimu walimuunga mkono na wengine hawakumuunga mkono hivyo ikasababisha Walimu takribani 7 kuihama shule hiyo kwa muda wa miezi miwili hadi mitatu‘ – DC Mgandilwa

Ukitaka kupata kila alichosema naomba bonyeza play hapa chini kumsikiliza kwa urefu

VIDEO: Matokeo ya Form IV yametoka, huyu ndio Mwanafunzi aliefaulu zaidi, tazama alivyopokewa shuleni kwao na alichokiongea.

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement