Tangaza Hapa Ad

AyoTV

VIDEO: Mengine yakufahamu kuhusu FlyEmirates

on

Shirika la ndege la Emirates linasifika kuwa na ndege za gharama na kifahari sana duniani ambapo wanasema kuwa wana ndege za abiria 235 na ndege 15 kwa ajili ya kuchukua mizigo na bado wanaendelea kuagiza ndege zingine kutokana na uhitaji uliopo.

Kulingana na takwimu za mwaka 2014 wameweza kufungua matawi mengine duniani ikiwemo ya ndege za mizigo na jumla ya destinations wanazotembelea ni 155 katika nchi 81.

Licha ndege hizo kuwa na uwezo wa kusafirisha watu wengi kwa wakati mmoja yako mazuri mengine kwa upande wa Entertainment ambapo unaposafiri na ndege za Emirates unaweza kuangalia zaidi ya channel 2200, zaidi ya movies 500 kutoka duniani kote, kuna zaidi ya channel za muziki zaidi ya 1000, kuna video games zaidi ya 100 na pia unaweza ukatumia USB yako kuangalia movies au kusoma documents zako.

Akizungumza na Ayo TV na millardayo.com, Mhudumu wa Ndege za Emirates, Theresia Sudi amesema…….

>>>’Emirates in offer value for money services ambayo unaona faida ya kutumia pesa zako unaponunua tiketi yako kuanzia unapotoka nyumbani mpaka unapofika sehemu unayokwenda, tuna uwezo wa kukuunganisha kwa haraka, hauna haja ya kusubiri sana airport kwa mfano unatoka Tanzania unafika pale Dubai kwa sababu tuna ndege nyingi tuna uwezo wa kukuunganisha kwa haraka zaidi’

>>>’Katika ndege za Emirates una uwezo wa kuonana na wahudumu wa Emirates ambao wamechaguliwa katika nchi 130 duniani na wanaongea lugha zaidi ya 60, hawa ni pamoja na watanzania kwa hiyo unaweza ukampata mtu anayeongea lugha yako’:-Theresia Sudi

Una uwezo wa kuangalia video hii hapa chini

ULIKOSA YA BEN POL VS JUX KWENYE JUKWAA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Tupia Comments

Advertisement