Tangaza Hapa Ad

Mix

MSIBA: Mke wa Waziri wa Habari Dkt. Harrison Mwakyembe amefariki

on

Taarifa zilizonifikia asubuhi hii ni kuhusu kifo cha mke wa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dr. Harrison MwakyembeLinah George Mwakyembe aliyefariki usiku wa July 15, 2017 katika Hospitali ya Aga Khan, Dar es salaam.

Linah alikuwa amelazwa katika Hospitali hiyo akipatiwa matibabu ambapo toka July 7 ndio Watanzania wengi walifahamu kuhusu kuumwa kwake baada ya Waziri Mwakyembe kuhudhuria tamasha la Saida Karoli na kusema “mke wangu yuko ICU lakini nimemuomba ruhusa nije kukuunga mkono Saida Karoli”

Shughuli za msiba zinafayika nyumbani kwake Kunduchi Beach, Dar es salaam, Ayo TV na millardayo.com zinaungana na Watanzania wote kumpa pole Waziri Mwakyembe katika kipindi hiki kigumu, Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.

VIDEO: “Mke wangu yuko ICU lakini nimekuja kwa Saida Karoli” – Waziri Mwakyembe

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement