Airtel TZ - Ad
Ads Separator
Startimes Ad
Home » Entertainment » The Game aweka wazi kuhusu uhusiano wake na Kim & Khloe Kardashian

January Makamba - Tanzania Mpya

The Game aweka wazi kuhusu uhusiano wake na Kim & Khloe Kardashian

gameKhloe Kardashian na The game walijiachia pamoja kwenye night club kiasi cha kuwapa watu mashaka kwamba  wawili hao wapo kwenye uhusiano wa kimapenzi hivi sasa.

Khloe alikuwa wa kwanza kukanusha uhusiano huo na kusema kwamba walikuwa wapo kwenye starehe kama marafiki.

Hivi karibuni The game amepata nafasi ya kuzungumzia kuhusu kile kilichotokea na ametoa exclusive mpya.

Akiwa kwenye radio ya BBC Radio1 Extra The game alisema asingeweza kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Khloe kwasababu alikuwa na uhusiano na dada yake Kim kipindi kilichopita.

“Watu hawajui kuhusu mimi na Khloe kwamba tumejuana miaka 12 iliyopita. Nilikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Kim Kardashian kwa muda kidogo sana. Kanye West alikuwa bado mshkaji kipindi kile na hadi sasa bado ni mshkaji wangu na najua Kim anakaribia kuwa mke wake na tayari wanafamilia. Khloe pia ni mshkaji na tuko poa pamoja kwa hiyo hizo tetesi  kati yangu na Khloe hazina ukweli”

k

Tags :
Previous post link
Next post link
Scroll To Top