AyoTV

Bondia Hassan Mwakinyo amedai dili lake na Mayweather limeingiliwa na madalali

on

Bondia Hassan Mwakinyo baada ya kufanikiwa kufanya vizuri katika mchezo wa ngumi hivi karibuni, leo amepata dili la miaka mitatu la kuwa balozi wa kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa.

Mwakinyo baada ya kutangazwa kuingia mkataba wa ubalozi wa miaka mitatu, alifunguka kuhusiana na madai yake ya kuhitaji pambano na mabondia wakubwa kama Floyd Mayweather.
Leo Mwakinyo amesema malengo yake sio kuwa chini ya Mayweather au The Money Team (TMT) ya Mayweather  ila malengo yake ni kupata pambano na bondia huyo ila kwa bahati mbaya madalali wameingilia kati dili hilo.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri bondia Hassan Mwakinyo alijizolea umaarufu mkubwa mwezi September 2018 baada ya kumpiga bondia muingereza Sam Eggington kwa kumpiga Technical Knock Out  round ya 2 katika pambano la round 10.


“Tumeshinda ili kuweka tabasamu usoni kwa MO Dewji”-Kocha Simba SC

Soma na hizi

Tupia Comments