Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Sasa Chris Brown na mzazi mwenza wako sawa kuhusu malezi ya mtoto wao

on

Inaripotiwa kuwa mwimbaji wa miondoko ya RnB Chris Brown pamoja na mzazi mwenzake Nia Guzman kwa sasa wapo kwenye maelewano mazuri ya kumlea mtoto wao Royalty baada ya kuwa na mvutano mkubwa kwenye suala la malezi miezi kadhaa iliyopita.

Nia Guzman ambaye ni mama mzazi wa Royalty amekanusha taarifa ambazo zimekua zikisambaa kuhusu kudai pesa za malezi ya mtoto huyo mwenye umri wa miaka mitano kutoka kwa Chris Brown na amethibitisha kuwa kwa sasa wapo kwenye maelewano mazuri.

Kwa mujibu wa mtandao wa The Blast uliandika kuwa mwezi February CB alitakiwa kutoa kiasi cha zaidi ya shilingi Mil.40 za Kitanzania  kwa ajili ya malezi ya mtoto wao lakini hakufanya hivyo, hata hivyo Nia Guzman amekanusha taarifa hizo na kusema walimaliza kesi yao vizuri.

Ikumbukwe kuwa mwaka 2017 Nia Guzman alifungua mashtaka dhidi ya Chris Brown kuhusu malezi ya mtoto wao lakini baadae Mahakama ya California nchini Marekani ilitupilia mbali kesi hiyo.

VIDEO: MISS ARUSHA AANGUA KILIO JUKWAANI

Soma na hizi

Tupia Comments