Tangaza Hapa Ad

HekaHeka

HEKAHEKA: Hatua zilizochukuliwa kwa aliyemtoboa Macho kijana Buguruni DSM

on

Jana September 29, 2016 Millardayo.com ilikuletea Hekaheka ya kijana mmoja kutoka Mabibo Hostel jijini Dar es salaam aliyetobolewa Macho na mtu aliyefahamika kwa jina la Scorpion ambaye kwa mujibu wa maelezo ya kijana huyo ilidaiwa kuwa anaogopwa sana kutokana na historia ya matukio aliyokuwa akiyafanya mara kwa mara.

Leo September 30, 2016 Heka Heka ya Leo Tena kupitia Clouds FM imefuatilia mkasa huo kiundani zaidi baada ya Geah Habib kufika Buguruni na kuzungumza na wananchi wa eneo hilo na wengine kukiri kushuhudia tukio alilofanyiwa kijana huyo lakini walishindwa kutoa msaada kwasababu tu Scorpion alikuwa na uwezo wa kumdhuru mtu na hatua zisichukuliwe juu yake. 

>>>’Watu wote wanamuogopa hawakuthubutu kusogea wala kumtetea inasemekana hili ni tukio lake la tatu…… ila sisi tuna hofu hatuna amani yule akikutamani umekishwa kwa sababu yeye anavyokufuata watu wote watabaki kuangalia tu huna mtetezi mpaka jama atakapo jiridhisha:Mkazi Buguruni

>>>Ni kweli hilo tukio limetokea na polisi tayari walishachukua hatua kwa maana ya huyo mtuhumiwa Scorpion jina lake halisi anaitwa Salum Mpepe alikamatwa siku ya tarehe 12 mwezi wa 9 akawa pale kituo cha polisi Buguruni wakati upelelezi ukiendelea tarehe 23 mwezi wa 9 alifikishwa mahakami na kusomewa jinai namba 276 unyang’anyi kwa kutumia silaha, yupo magereza kesi yake itatajwa tena tarehe 5 mwezi wa 10 2016:- Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Salum Hamdani.

KUSIKILIZA FULL STORI UNAWEZA KUBONYEZA PLAY HAPA CHINI

ULIPITWA NA KAULI YA MWENYEKITI WA CHADEMA FREEMAN MBOWE KUHUSU UKUTA OCTOBER 1? TAZAMA HAPA

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement