Tangaza Hapa Ad

HekaHeka

Ufafanuzi kuhusu Kondakta aliyedaiwa kuuawa na Wanajeshi kwa kipigo Tanga

on

Kwenye hekaheka ya leo January 31 2016, Geah Habib ametuletea hekaheka kutokea Tanga inayohusu Kondakta aliyedaiwa kuuawa na wanajeshi kwa kipigo.

Taarifa zinadai kisa chenyewe kilianzia kwa Msichana ambaye ni mtoto wa Mwanajeshi kupanda Daladala bila kulipa nauli hivyo Kondakta akachukua maamuzi ya kuchukua begi lake mpaka alipe nauli ambapo baada Msichana huyo alikwenda kushtaki kwa baba yake.

Inadawai Baba wa huyo mtoto alituma vijana wake waifuatilie gari hiyo na ilipopita kondakta alishushwa na akaingizwa ndani ya kambi ya jeshi wakampiga mpaka hali yake ikawa mbaya, alirudishwa nyumbani na wakati anapelekwa hospitali alifariki.

Ufafanuzi umetolewa na kamanda wa polisi Tanga, Benedict Wakulyamba kuhusu tukio hilo kwa kuzungumza yafuatayo >>> ‘Zimekuwepo taarifa kwamba waliompiga ni Wanajeshi, kwa hatua tuliyoifikia ya kuwakamata baadhi ya watuhumiwa hakuna Mwanajeshi aliyehusika moja kwa moja japo lilifanyikia kwenye kambi ya jeshi’

Unaweza kubonyeza play hapa chini kupata taarifa yote

Ulikosa? undani wa ishu ya Mke kuwamwagia mafuta ya moto Mume na Mtoto? Bonyeza play hapa chini kusikiliza

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement