HekaHeka

HEKAHEKA: Cheti cha kuzaliwa chafichua siri ya mtoto

on

Kwenye Leo Tena ya Clouds FM leo October 11, 2017 Mtangazaji Geah Habib ameifikisha Hekaheka iliyotokea Keko Dar Es Salaam baada ya mdada mmoja ambaye aliolewa na kukuta mtoto wa mume wake akilelewa na mama mkwe wake bila kujua kuwa mtoto huyo sio wa familia hiyo.

Inasemakana mtoto huyo amelelewa na bibi ambaye sio bibi yake halali pamoja na mama wa kambo toka akiwa na miaka miwili na kusomeshwa mpaka kufikia darasa la tano na baadae kugundulika kuwa mtoto huyo sio  mjukuu wa yule bibi wala baba aliyedaiwa kuwa baba yake mzazi na baadae kurudishwa kwa baba yake mzazi ambae  ni dereva bajaji, hiyo ni baada ya kupata cheti cha kuzaliwa cha mtoto huyo.

HEKAHEKA: Kaburi la maajabu Tanangozi Iringa

Soma na hizi

Tupia Comments