Tangaza Hapa Ad

Mix

Idriss ashindwa kuvumilia na kuyaandika haya, imeanzia kwa sauti ya Wema Sepetu

on

Mchekeshaji/Mtangazaji na Mshindi wa Big brother Africa Idriss Sultan ameonyesha kutofurahishwa na sauti iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikiwa inasikika sauti ya Wema Sepetu akitoa malalamiko yake na kuzungumzia ishu ya kukamatwa kwake na Polisi.

Inaonekana sauti hizo zimerekodiwa bila Wema Sepetu kufahamu kama anarekodiwa hivyo akajiachia akijua anaongea maongezi ya faragha na waliokwenda kumtembelea.

“Na muendelee kupiga kelele kutembelea watu central na kuwarekodi bila wao kujua kwakua tunachukulia maisha ya watu kama mfumo wa likes na following bila kujua tunawaumiza kiasi gani kwa tunachokifanya’

“Basi tuendelee na tutaona kama tunaowapenda kama tunavyosema tutakua tumewatendea haki, kwa hili nimeshindwa kunyamaza, mnajidai Marafiki na watu wa kweli  kumbe unafki unatujaa’

“Tutaua Familia zetu na kuwa wa kwanza kulia kwenye msiba, UBINADAMU UKWAPI ? ? Kama hamjaenda kutoa moral support basi kaeni majumbani kwenu na mposti posti vimachozi na unafki wenu sio kutuchafulia hata pale pasafi padogo palipobaki ???”

VIDEO: Maagizo matatu ya Paul Makonda kwa kila mzazi Dar es saalaam na mengine, tazama kwenye hii video hapa chini

VIDEO: Wema Sepetu, T.I. na wengine walivyoingia Polisi kutii wito wa Paul Makonda, tazama kwenye hii video hapa chini

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement