Tangaza Hapa Ad

Magazeti

Kachumbari yasababisha Mume kumuua Mke Tanzania

on

Kila asubuhi mimi Millard Ayo nazisogeza karibu yako habari zote kubwa kutoka kwenye Magazeti mbalimbali ya Tanzania ambapo huwa naziweka kwenye page ya Twitter ya @millardayo na kwenye Youtube ya millardayo na millardayo.com.

Moja ya habari iliyoandikwa kwenye magazeti ya leo January 20 2017 ni pamoja na hii ya kwenye gazeti la Mtanzania, yenye kichwa cha habari ‘Mume aua mke kisa kachumbari’ 

Gazeti hilo limeripoti kuwa mkazi wa Mtaa wa Mageuzi, Manispaa ya Shinyanga, Stella Ibrahim (39), anadaiwa kuuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na mume wake, Ibrahim Daniel kwa kile kilichoelezwa  kuwa alipewa kachumbari iliyochacha.

Tukio hilo limetokea juzi usiku, baada ya Daniel kumshushia kipigo mkewe akidai kuwa alimpa kachumbari ambayo haikuhifadhiwa vizuri na mboga nyingine aliyodai haina kiwango.

Mashuhuda wa tukio hilo, walidai kuwa Daniel alifika nyumbani akiwa amelewa, kisha kuulizia  kachumbari ambayo alikula jana, ndipo mtoto wake, Elizabeth Ibrahim (13) akamwonesha kachumbari  ambayo inadaiwa tayari ilikuwa imechacha.

Walisema hakufurahia kuona kachumbari hiyo imeharibika, ndipo alipoanza kuuliza kwanini haikuhifadhiwa vizuri, akisimulia mkasa huo, mtoto wa marehemu, Daniel Ibrahim (12) alisema baba yeke alifika nyumbani saa moja usiku, alimkuta yeye akiwa na mdogo wake, Elizabeth aliyemuhoji kwanini kachumbari imeharibika, lakini hakupata jibu.

‘Baada ya kuingia ndani, baba alimuuliza Elizabeth kachumbari aliyoiacha (Januari 16, mwaka huu) iko wapi, akaoneshwa. Baada ya kuiangalia aliiona imechacha, alitoka nje na kuchukua fimbo ambayo huwa anaiweka juu ya nyumba na kutaka kuanza kumpiga, kabla ya kuanza kumpiga Elizabeth alikimbia.;-Mtoto wa marehemu

“Baada ya Elizabeth kukimbia, mama ambaye alikuwa kazini alifika nyumbani, akamkuta baba akifoka, akauliza kuna nini, baba akasema kwanini hakupika mboga yenye kiwango na kwanini ulipikwa ugali mwingine wakati  kulikuwa na ugali uliobaki mchana’;- Mtoto wa marehemu 

Alisema kutokana na maswali hayo, mama yake alimjibu kwa hasira kwanini hakuacha fedha nyumbani za kununulia mboga yenye kiwango anachotaka.

Baada ya baba anayedaiwa alikuwa amelewa kudai kachumbari yake, mama aliingilia kati, akajikuta anaambulia kipigo… vipimo vya daktari vinaonyesha alipigwa na kitu kizito kwenye utosi, kichwa kikavimba na damu kavujia ndani kwa wingi’;-Mwenyekiti wa mtaa

AyoTV MAGAZETI: Vilio Mgodi mkubwa nchini kufungwa,Wanaosoma diploma kupewa mikopo, Bonyeza play hapa chini 

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement