Tangaza Hapa Ad

Magazeti

Polisi washtukia mbinu mpya ya ‘wauza unga’

on

Kila asubuhi Millard Ayo atazisogeza karibu yako habari zote kubwa kutoka kwenye Magazeti mbalimbali ya Tanzania ambapo huwa naziweka kwenye page ya Twitter ya @millardayo na kwenye Youtube ya millardayo bila kusahau millardayo.com.

Moja ya habari iliyoandikwa leo January 10 2017 ni pamoja na hii ya gazeti la Mwananchi yenye kichwa cha habari Polisi washtukia mbinu mpya ya ‘wauza unga’

Gazeti la Mwananchi limeripoti kuwa wafanyabiashara wa dawa za kulevya wamebuni mbinu mpya kwa kusafirisha na kuingiza nchini, vibashirifu (kemikali zinazotumika kutengeneza dawa ya kifua) aina ya ephedrine kisha kuvitumia kutengeneza cocaine na Heroin.

Kamanda wa polisi, kikosi cha dawa za kulevya, Mihayo Msikhela amesema kwamba wafanyabiashara hao usafirisha kemikali hizo kutoka bara la Asia na wanapozifikisha nchini hutumia kutengeneza dawa hizo za kulevya.

Kadhalika amesema wafanyabiashara hao hununua kemikali hizo bila kuwa na kibali cha serikali na hudanganya na hudanganya kuwa zitatumika kutengeneza dawa za kifua.

Nimekuwekea hapa nyingine 10 kubwa zilizoandikwa na magazeti ya Tanzania leo January 10 2017

AyoTVMAGAZETI: Hatimaye fedha kurudi mtaani, Serikali yashtuka ubia na shule za masingi, Bonyeza play hapa chini

Unazitaka Breaking NEWS na Stori zote? ungana na Millard Ayo kwenye Facebook Twitter Instagram na Youtube na atakuletea matukio yote ya picha, video na habari iwe usiku au mchana…. bonyeza hapa >>> FB Twitter Instagram YouTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement