Tangaza Hapa Ad

Mix

Wafungwa wauawa ndani ya gereza Brazil

on

Taarifa iliyoripotiwa leo January 15 2017 na vyombo mbalimbali vya kimataifa zimedai kuwa polisi wa kukabiliana na ghasia Brazil wanajaribu kila wawezavyo kuingia ndani ya gereza kuu katika jimbo la Rio Grande do Norte, ambalo limetwaliwa na wafungwa.

Idara ya polisi inasema kuwa zaidi ya wafungwa kumi wameuwawa, baadhi yao kwa kukatwa katwa katika makabiliano makali kati ya magenge hasimu katika gereza hilo la Alcaçuz. Polisi hao wamefika nje ya ukuta wa gereza hilo wakisubiri hadi kutakapopambazuka ndipo waingie ndani.

Mwaka jana pekee zaidi ya wafungwa 100 walifariki katika makabiliano kama hayo nchini humo katika magereza yaliyoko katika majimbo ya Amazonas na Roraima.

AyoTVMAGAZETI: Simulizi ya maisha ya Lema gereza la Kisongo, Ufisadi polisi wafikia kwa DPP, Bonyeza play hapa chini 

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement