Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Maneno ya Naibu Waziri wa Afya shabiki namba 1 wa Fid Q

on

Muziki wa Bongofleva unaendelea kufanya vizuri na sasa hivi imekua sio ajabu sana kuona viongozi mbalimbali wa Tanzania wakitoa saluti za kutosha kwa vijana wa Kitanzania waliojiajiri kwenye sanaa.

Naibu Waziri wa Afya Dr. Hamis Kigwangalla hajaficha ushabiki wake kwa kusema yeye ni miongoni mwa wanaomfatilia kwa sana mwanahiphop Fid Q na mistari yake iliyo deep.

Naibu Waziri Kigwangala.

Kupitia Twitter page yake Kigwangalla ameonyesha kuielewa pia ngoma mpya ya Fid Q aliyoachia leo, akaandika >>>Huwa nasikiliza wasanii wachache sana wa Bongofleva, ni mmojawao sababu anajua kutunga mistari na ana attitude ya hip-hop!

Kwenye tweet nyingine akaandika sehemu ya mistari ya ngoma mpya ya Fareed >>’wengi wana-cheat na kuwaudhi wachache wanao-play fair!” nimeiba mstari huo kwenye ukurasa wa Makonda kule IG, nimeielewa hii namba’ baada ya maneno hayo akaweka alama ya kunyoosha mikono juu.

ULIPITWA? Maswali Alikiba na Ommy Dimpoz waliyoulizana yako hapa chini kwenye hii video

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement