Tangaza Hapa Ad

Mix

VIDEO: Taarifa ya Jeshi la Polisi kuhusu miili 7 Mto Ruvu na kupotea kwa Ben Saanane

on

Leo December 21, 2016 Jeshi la Polisi Makao Makuu limetoa taarifa kupitia kwa Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kamishna Robert Boaz juu ya kupatikana kwa miili ya watu 6 eneo la mto Ruvu pamoja na kupotea kwa Ben Saanane ambaye ni msaidizi wa mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe.

Katika taarifa yake, Kamishna Boaz amesema polisi walipokea taarifa za kupotea kwa Ben Saanane mnamo December 5 2016 na tayari jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili kubaini mahali alipo kiongozi huyo kutoka chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema.

Aidha jeshi hilo limetoa ufafanuzi kuhusu kupatikana kwa miili sita ya watu iliyookotwa ikiwa kwenye maguni pembezoni mwa mto Ruvu, Jeshi la polisi limesema kuwa bado wanaendelea na uchunguzi ili kufahamu watu hao ni akina nani ni sababu zipi zilizopelekea kifo chao.

VIDEO: Upo hapa ufafanuzi wa Jeshi la Polisi kuhusu mtu aliyefariki baada ya kubaatizwa. Tazama video hii

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement