PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Breaking News

BREAKING: Lazaro Nyalandu amjibu Kigwangalla, amuandikia sentensi 7

on

Leo mchana November 13, 2017  Waziri wa Maliasili na Utalii Dr Hamisi Kigwangalla aliliagiza Jeshi la Polisi pamoja na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU kuanza kumchunguza mara moja Lazaro Nyalandu alikua Waziri wa wizara hiyo kwenye awamu iliyopita.

Baada ya kauli hiyo, Lazaro Nyalandu ametumia muda wake kumjibu Kigwangalla leo na kuandika yafuatayo….

INASIKITISHA sana kuona WAZIRI Kigwangalla akitumia MUDA wake ndani ya BUNGE leo kunichafua, kunidhihaki, na kusema UONGO na UZUSHI dhidi yangu, ikiwa ni NJAMA za makusudi zilizopangwa kunichafua mara baada ya mimi kukihama Chama Cha Mapinduzi -CCM.

Aidha, hatua hiyo imepangwa kwa lengo la kuhakikisha kuwa hakuna kiongozi yeyote wa CCM atakayethubutu ama kudiriki tena kukihama Chama Cha Mapinduzi CCM katika Serikali hii ya awali ya tano. AIDHA, Waziri Kigwangalla anatumika VIBAYA, kwa kauli za UONGO na UZUSHI aliuanza DHIDI yangu mara tu alipoteuliwa, kwa kuanza kutoa kauli za kejeli dhidi ya UTUMISHI wangu uliotukuka ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii na wenye REKODI thabiti.

NIANZE na UZUSHI alioutoa Waziri Kigwangalla mapema leo BUNGENI, huku moyoni mwake akiwa anajua fika kuwa ametumwa kusema UONGO dhidi ya Waziri Nyalandu kwa lengo la kuandaa MAZINGIRA ya kumkamata na kubwa zaidi, kudhalilisha azma ya WATANZANIA ambao WAKO tayari kwa mabadiliko ya UONGOZI wa nchi kupitia UPINZANI.

AIDHA, propaganda za Kigwangalla ameamua zimuhusu Waziri mmoja tu wa Maliasili, tangu TAIFA kupata Uhuru. Waziri huyu ni Nyalandu, ambaye wala sio Waziri ambaye yeye amemrithi alipoteuliwa kuwa WAZIRI, jambo linalothibitisha NJAMA na Progaganda za kuzimisha MOTO na nguvu ya umma kupitia UPINZANI, hasa baada ya kitendo changu Cha kukihama CCM.

1) WAZIRI Kigwangalla amekejeli kuwa Waziri Nyalandu alitumia Fedha za Serikali kusafiri USA na mwanadada Aunt Ezekiel. -HABARI hii ilikuwa ya KUZUSHA na ilichunguzwa na vyombo vya dola 2014 na kuthibitika ilitungwa na ilikuwa ya UONGO.

Katika Mkutano huo wa Washington, DC, Waziri Nyalandu alialikwa na Balozi wa Tanzania, Marekani, na alipewa RUHUSA ya maandishi na Serikali kuhutubia Mkutano huo kwa siku Moja. Wasanii wote Walioalikwa, akiwepo Mwanadada Aunt Ezekiel, hawakuwa na mwaliko wa Wizara ama Serikali, bali waandaji wa Kongamano. Na Serikali haikulipa gharama zozote kwao.(Mthibiti
Na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali anaweza kuthibitisha)

2) Waziri Kigwangalla amedanganya BUNGE kuwa Waziri Nyalandu alitumia helikopta kugombea URAIS 2015.
-Habari hii ni ya uzushi na UONGO, na Waziri atakuwa aidha hana BUSARA 

ULIKOSA? Nyalandu kuanza kuchunguzwa na TAKUKURU na Polisi, Kigwangalla aagiza? Bonyeza play hapa chini kutazama

FREEMAN MBOWE NOV 12 2017: “SIMUOGOPI YEYOTE, LIPUMBA NI PROFESA WA AJABU KWELIKWELI” BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA

IMEFAHAMIKA: HAPA NDIPO ANAPOISHI DR. LUIS SHIKA, MAJIRANI WAONGEA… BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA MWANZO MWISHO

Soma na hizi

Tupia Comments