PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Michezo

Humud kajibu tuhuma za kudaiwa kutembea na wake wa wachezaji wenzake

on

Baada ya Club ya KMC ya Kinondoni kutoa taarifa za kuvunja mkataba na kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania na club za Simba na Azam FC Abdulahim Humud, leo mchezaji huyo ametoa tamko na ukweli wake kuhusiana na tuhuma hizo.

KMC walitangaza kuvunja mkataba na Abdulhalim Humud kwa sababu mbalimbali lakini mbele ya waandishi wa habari walizitaja sababu mbili ambazo ni utovu wa nidhamu na shutuma za kumtaka mpenzi wa mchezaji mwenzake (Room mate)

Humud leo amejibu tuhuma hizo na kusema kuwa sio za kweli na zinalenga kumchafua katika soka, Humud ameeleza kuwa yeye ndio aliomba aachwe kutokana na kukosa nafasi ya kucheza, Humud amefika mbali zaidi na kusema kuwa kukosa kwake kucheza ni kutokana na kukataa kugawana parcent za mshahara na dau la usajili wake na baadhi ya watu.

Hakuna anayemkuta Samatta kwa sasa Jupiter Pro League 2018/19

Soma na hizi

Tupia Comments