Michezo

Matokeo ya Kombe la FA kwa mechi za leo.

on

arssenal

Mzunguko wa nne wa mashindano ya kombe la chama cha soka nchini England maarufu kama FA Cup umeanza hii leo kwa michezo kadhaa iliyopigwa kwenye viwanja mbalimbali nchini humo .

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa kwenye uwanja wa Ewood Park mabingwa wa ligi ya England kwa msimu wa mwaka 94/95 Blackburn Rovers ambao siku hizi wanacheza ligi daraja la kwanza Blackburn Rovers waliwabana Manchester City kwa kuwalazimisha  sare ya 1-1 .

 City ndio walioanza kufunga kupitia kwa mshambuliaji wa kimtaifa wa Hispania Alvaro Negredo kabla Blackburn hawajasawazisha kupitia kwa Scot Dunn .

Matokeo haya yanamaanisha kuwa timu hizi zitarudiana katika mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Manchester City wa Etihad katika tarehe itakayopangwa hapo baadaye.

Katika mchezo mwingine mkubwa wa mashindano hayo ya kombe la FA uliopigwa hii leo (Jumamosi) Arsenal wamewafunga watani wao wa jadi Tottenham Hotspurs kwa matokeo ya    2-0.

Mabao ya Arsenal kwenye mchezo huo yalifungwa na Santiago Cazorla na Tomas Rosicky.

Tupia Comments