Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Navy Kenzo waeleza furaha kutajwa kuwania MTV MAMA 2016

on

Sept 21, 2016 majina ya wasanii watakaowania tuzo za MTV MAMA 2016 yalitajwa huku Naseeb Abdul aka Diamond Platnumz na kundi la Navy Kenzo pamoja  na Alikiba ndio wasanii wa Tanzania waliotajwa kuwania tuzo kubwa za Africa za MTV Africa Music Awards 2016.

Sasa millardayo.com & Ayo TV imewapata Navy Kenzo huku wakayaongea haya>>>Tunashukuru sana tumepata taarifa za MTV MAMA 2016 tumechaguliwa kwenye Best Group yaani tumefurahia sana ni kitu ambacho kimetutia nguvu sana

Kimeonesha jinsi gani kazi yetu ambayo tuliyokuwa tukifanya kwa muda mrefu ndio imeanza kuleta matunda hayo kwahiyo tunashukuru sana, tutatoa maelekezo katika mitandao yetu ili mashabiki wetu na wengineo wajue jinsi ya kutupigia kura’

Unaweza ukabonyeza play kuwasikiliza Navy Kenzo furaha yao baada ya kutajwa kuwania MTV MAMA 2016

ULIIKOSA HII YA SAUTI SOL KUHUSU KUSAINISHA WASANII NA COLLABO YAO MPYA NA WEUSI BASI BONYEZA PLAY HAPA

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement