Tangaza Hapa Ad

Mix

Good News: Baada ya Multichoice kuanzisha Promotion, imewapata Washindi

on

Zawadi kutoka MULTICHOICE Tanzania zilikuwepo siku nyingi na kinachofanywa sasa ni muendelezo tu wa kilichoanzishwa ambapo mara nyingi tumeshuhudia jinsi wanavyowazawadia wateja wao.

Leo ni zamu ya Wateja 76 wa DStv ambao wamejinyakulia zawadi mbalimbali kutoka Multichoice Tanzania katika promosheni inayoendelea ya ‘Jishindie na DStv’ ambapo mteja hupata fursa ya kujishindia zawadi kwa kulipia king’amuzi chake kwa angalau miezi miwili mfululizo.

Afisa Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Abdallah (katikati waliokaa) akifuatilia droo ya kuchagua washindi wa promosheni ya Jishindie na DStv. Kulia ni Meneja Uhifadhi Wateja wa Multichoice Tanzania Hilda Nakajumo, Wengine ni Maafisa wa Multichoice Erick Mosha (aliyesimama) na Leyla Partick

Naambiwa Washindi 25 kati yao wamejipatia ving’amuzi vya DStv Explora ambavyo ni vya kisasa huku Washindi watatu wakijishindia Kifurushi cha Premium cha Tsh 184,000 cha mwezi mmoja, Washindi watatu wengine wameshinda Kifurushi cha Compact+ cha Tsh 122,500, huku Washindi 10 wakishinda kifurushi cha Compact cha Tsh 82,250.

Washindi 10 wengine wamejishindia Kifurushi cha Familia cha Tsh. 42,900 na Kundi la Washindi wengine 25 wamejishindia Kifurushi cha Bomba cha Tsh 19,975 huku Washindi hao wa droo ya kwanza wametoka kila pembe ya nchi ikiwemo Dar es Salaam, Kagera, Iringa, Geita, Kilimanjaro, Kigoma, Mbeya, Mwanza na Morogoro.

Unaambiwa Promosheni hii itaendelea kwa muda wa miezi miwili na itatoa washindi wa zawadi mbalimbali ikiwemo vifurushi vya muda wa matangazo, ving’amuzi, pamoja na zawadi kubwa kabisa ambayo ni safari ya Kitalii Visiwani Zanzibar kwa washindi wawili pamoja na familia zao.

Afisa Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Abdallah (kushoto) akifuatilia droo ya kuchagua washindi wa promosheni ya Jishindie na DStv. Katikati ni Meneja Uhifadhi Wateja wa Multichoice Tanzania Hilda Nakajumo na kulia ni Meneja wa Uendeshaji wa Multichoice Tanzania Baraka Shelukindo

Akizungumza baada ya kuchezeshwa kwa droo ya kwanza katika ofisi za Multichoice Tanzania, Meneja wa Uhifadhi Wateja Hilda Nakajumo amebainisha kuwa zaidi ya wateja Elfu 10 wameshiriki kwenye droo hiyo ikimaanisha ni muitikio mkubwa wa wateja na kuwataka waendelee kutumia huduma hiyo ili kuingia kwenye droo zitakazochezeshwa kila baada ya wiki mbili huku droo kubwa ya mwisho ikitarajiwa kufanyika September 1, 2017.

Tupia Comments

Advertisement