Tangaza Hapa Ad

Michezo

Muda atakaokaa nje ya uwanja Blagnon wa Simba baada ya kupasuka

on

Mshambuliaji wa kimaifa wa Ivory Coast anayeichezea klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba Fredrick Blagnon, Jumapili ya October 23 2016 alishindwa kumaliza mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Toto Africans ya Mwanza baada ya kuumia.

Blagnon alishindwa kuendelea na mchezo kufuatia kupasuka sehemu ya usoni iliyopo karibu na jicho, hiyo ilikuwa baada ya kugongana na mchezaji wa Toto Africans, Blagnon alitolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Laudit Mavugo.

dsc_0044

Leo October 23 daktari wa timu ya Simba Yassin Gembe amethibitisha kuwa staa huyo atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa siku 7 kufuatia kupasuka huko, ila baada ya siku tatu ataanza kufanya mazoezi yake binafsi ila baada ya siku saba ndio ataungana na wenzake kwenye mazoezi ya pamoja.

ALL GOALS: Yanga vs Simba October 1 2016, Full Time 1-1

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement