Habari za Mastaa

Meek Mill atoboa siri kuhusu Jay Z kipindi cha bifu lake na Drake (+video)

on

Rapper Meek Mill ametoa siri ambayo watu wengi hawaijui na kusema kuwa Jay Z aliwahi ku-play ngoma ya Drake ‘Back to Back’ kwa bahati mbaya kwenye mualiko alioupata kutoka kwa Jay Z na Beyonce kwenye chakula cha jioni pamoja na Nicki Minaj.

Ngoma ya ‘Back To Back’ ni miongoni mwa diss tracks za Drake kwa Meek Mill ambayo ilitoka mwaka 2015 kipindi cha bifu yao na wimbo huo unatajwa kuingia kwenye orodha ya diss kali za muda wote.

Meek Mill alitoa tamko na kusema inawezekana kufanya kazi pamoja na Drake, kauli hii inakuja baada ya wawili hao kumaliza tofauti zao September 2018 baada ya kuwa na bifu kwa muda mrefu.

“Nakumbuka nilikua na Nicki Minaj tukaitwa na Beyonce pamoja na Jay Z kwenye chakula cha usiku mara ghafla Jay Z aka-play ngoma ya ‘Back to Back’ Beyonce na Nicki walibaki wanaangaliana na sikumbuki kama wanakumbuka kitu kama hichi” >>>Meek Mill

EXCLUSIVE: CHALII YA CHUGA BENEFICIAL KAFUNGUKA “NI HUYO MIMI”

Soma na hizi

Tupia Comments