PremierBet Tanzania Usain Bonus Ad

Habari za Mastaa

Haya sasa!!! Davido aweka wazi siri ya mafanikio yake

on

Staa Davido ambaye pia ni mmiliki wa record label ya ‘Davido Music Worldwide’ ameamua kufunguka kwa mashabiki wake kuhusiana na siri ya utajiri alionao, Davido akiwa ni miongoni mwa mastaa wenye mafanikio makubwa Afrika.

Davido ametumia ukurasa wake wa instagram kutoa siri hiyo na kusema kuwa mara nyingi huwa anafanikiwa katika maisha kutokana na kuwapa watu wake wa karibu uwanja wakuwaona wakifanikiwa zaidi kuliko yeye na kuwaweka katika njia sahihi ya kuona mafanikio.

Staa huyo ameongezea na kusema kuwa haijalishi hata kama sio wakati wako wa kufanikiwa lakini wasaidie wengine wafanikiwe katika maisha na kumalizia kwa kusema kuwa hivyo ndivyo alivyo.

“Ninafanikiwa siku zote kwasababu nahakikisha mtu yeyote anayekuwa karibu yangu anafanikiwa au namuweka katika njia sahihi ya kufanikiwa, unatakiwa kuwaona watu wengine wakifanikiwa hata kama sio msimu wako wa mafanikio”

Jionee Jengo refu DSM, apartment zake simchezo zinaanzia Million 250

Soma na hizi

Tupia Comments