Tangaza Hapa Ad

Mix

VIDEO: Polisi Makao makuu kuhusu tuhuma za rushwa dhidi ya Kamanda Sirro

on

Baada ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kudai mbele ya Waziri Mkuu kuwa Wafanyabiashara wa shisha walitaka kumhonga ili asipige kelele kuhusu Shisha kuendelea kuuzwa Dar es salaam, Polisi makao makuu wametoa tamko

Tamko hilo limetokana na Paul Makonda kumtuhumu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Simon Sirro na Kamanda Kaganda kuwa hawajachukua maamuzi na kwamba walimjibu shisha haipo tena Dar lakini yeye alivyofanya uchunguzi akakamata maeneo zaidi ya 10 hivyo akadai kuwa huenda wale waliomfuata kumhonga walipita kwa Polisi.

Kaimu Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai, CP Robert Boaz kutoka Makao makuu ya Polisi amesema tuhuma hizo wamezipokea na wanafanya uchunguzi.

>>>‘Hili linachunguzwa na kuna taasisi maalum zinazoshughulika na masuala ya rushwa na sisi tumepokea kama tuhuma, kwa mujibu wa taratibu zetu tuhuma zozote zile zinazotolewa dhidi ya kiongozi au Askari huwa inachunguzwa kwa hiyo tunachunguza’ 

AUDIO; Majibu ya RC Makonda kuhusu kauli zake zilizoibua maswali 

USIPITWE NA HABARI !!!!! Kazi ya Millard Ayo ni kukusogezea karibu habari zote kuanzia za Mastaa, burudani, michezo, siasa na mengine ya mtaa, jiunge na mimi kwenye Instagram, Facebook na Twitter kwa jina hilohilo la @millardayo kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM FACEBOOK TWITTER

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement