Tangaza Hapa Ad

Michezo

Staa aliyetua London kukamilisha usajili wake Arsenal

on

Mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania anayeichezea klabu ya Deportivo La Coruna Lucas Perez leo August 29 2016 amepigwa picha akiwa katika uwanja wa ndege wa Heathrow uliyopo London akiripotiwa kuelekea kukamilisha dili lake na Arsenal.

37B01ABA00000578-3763845-image-a-27_1472489518865

Lucas Perez alianza kuripotiwa na Sportsmail ijumaa iliyopita kuwa alikuwa London na tayari alishafanyiwa vipimo vya afya ndani ya Arsenal, hivyo dili lililokuwa limebakia ni kusaini mkataba wa kujiunga na Arsenal tu leo.

37B0127700000578-3763845-image-m-22_1472489480778

Staa huyo ambaye ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa wanaounda safu imara ya ushambuliaji ya Deportivo La Coruna, anaripotiwa kukaribia kujiunga na Arsenal kwa dau la usajili la pound milioni 17, hivyo kuonekana kwake leo katika uwanja wa ndege wa Heathrow inatajwa kuwa ndio anaenda kukamilisha dili lake Arsenal.

GOAL AND HIGHLIGHTS: YANGA VS TP MAZEMBE JUNE 28 2016, FULL TIME 0-1

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement