DSTV


Tangaza Hapa Ad

Michezo

Arsene Wenger amezipata taarifa za mchezaji bora wa dunia kuwa Rais Liberia

on

Moja kati ya habari zilizochukuwa headlines leo Alhamisi ya October 12 2017 ni kuhusiana na mchezaji bora wa dunia wa mwaka 1995 George Weah kushinda kiti cha Urais nchini Liberia.

Ushindi wa George Weah kuwa Rais wa nchi yake ya Liberia unampa heshima nyingine tena baada ya kuwa mchezaji pekee hadi sasa kutokea Afrika aliyewahi kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Dunia maarufu kama Ballon d’Or 1995.

George Weah ambaye amewahi kuvichezea vilabu vya AC Milan, Chelsea na Man City ameshinda Urais na kocha wa Arsenal Arsene Wenger amempongeza leo mbele ya waandishi wa habari.

George Weah alikuwa miongoni mwa wagombe wa Urais 20.

Wenger aliwahi kumfundisha Weah akiwa Monaco miaka ya 1990’s “Ningependa kumpongeza mchezaji wangu wa zamani kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Liberia, hutokea kwa nadra sana kuona mchezaji wa zamani anaweza kuwa Rais wa nchi, hongera sana George”

Kocha Wenger

List ya majina 30 ya wanaowania tuzo ya Ballon d’Or 2017

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement