Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Top Stories

Alichokiongea RUNGWE baada ya Lowassa kwenda Ikulu kwa JPM

on

Kumekuwa  na maneno mengi kutoka kwa viongozi mbalimbali na baadhi ya watu ambayo yamekuwa yakiendelea kupitia mitandao ya kijamii kuhusu aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa zamani na Mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA Edward Lowassa kwenda Ikulu na kuusifia utendaji kazi wa Rais Magufuli.

Leo Jan 13 2018 AyoTV imefanya Exclusive Interview na Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Hashimu Rungwe na kuelezea mtazamo wake kwa Lowassa kwenda Ikulu.

‘Mimi sikuona matatizo pale, lakini ilibidi wale watu wote wanaolalamika wangemngoja Lowassa akaja, pengine kamati kuu ya chama au halmashauri kuu ya chama itamuita yule mtu  na bila shaka Mwenyekiti alishasema yale aliyoyaongea si mambo ya chama ni mambo yake binafsi’- Hashimu Rungwe

‘Halafu katika chama ataeleza alichokwenda kama alitumwa na chama, atawaeleza mambo aliyoyolazimisha pale na  yapi wamekubaliana na yapi wamepeana ahadi, halafu kelele hizo ziishe, lakini kurukia na kulaumu sio ustaarabu na haileti picha nzuri,”-Hashimu Rungwe 

“Lowassa, umeikosea Tanzania”- Lema baada ya Lowassa kuipongeza Serikali

 

 

 

Soma na hizi

Tupia Comments