Tangaza Hapa Ad

AyoTV

VIDEO: ‘Maamuzi niliyoyatoa bungeni mengine yalikuwa hayanipendezi hata mimi’- Dr. Tulia Ackson

on

Najua kuna watu wangu wengi wamemfahamu Naibu spika Dr. Tulia Ackson zaidi katika mkutano wa tatu wa bunge la 11 ambapo headline nyingi ziliandikwa dhidi yake ikiwemo ishu ya wabunge wa upinzani kususia sehemu ya mkutano huo kwa madai hakuwa akitenda haki.

Lakini kuna baadhi ya mambo yawezekana kabisa ukatamani kuyajua kutoka kwake mfano ukikutana na Dr. Tulia mwenyewe ukamuuliza kama alishawahi kujutia maamuzi yoyote aliyowahi kuyafanya akiwa kwenye kiti majibu yake yatakuwa haya….

Hapana kwasababu mara nyingi nimekuwa nikifanya maamuzi kulingana na kanuni, kwahivyo maamuzi yote niliyokuwa nikifanya yaweza kuwa hayanipendezi hata mimi lakini kwa mujibu wa kanuni ni lazima yafanywe‘ –Dr. Tulia Ackson

Aidha ukimuuliza alikuwa anajisikiaje wabunge wa upinzani kususia vikao? Dr.Tulia ameyajibu haya..>>>’Wabunge kutoka ni jambo la kawaida lakini lile lilikuwa la ajabu kwa sababu wanatoka wote kwa pamoja, ningetamani wabaki lakini ni misimamo ya vyama kushughulika na wabunge wake‘ –Dr. Tulia Ackson

Wapo waliokuwa wanapenda kuendelea kubaki ndani ya bunge lakini hawakuweza kwavile akitoka anaweza akanyang’anywa kadi yake‘ – Dr. Tulia Ackson

Unaweza kuendelea kumsikiliza Dr. Tulia Ackson kwenye hii video hapa chini…

ULIZIKOSA DAKIKA 7 ZA NAIBU SPIKA DR. TULIA KUHUSU HISTORIA YA SAMUEL SITTA

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement