Habari za Mastaa

Kampuni ya Fendi waandaa show ya kumuaga Karl Lagerfeld (+video)

on

Kampuni ya mitindo ya Fendi ya nchini Italy imemuaga Mfalme wa masuala ya Fashion Karl Lagerfeld aliyefariki February 19,2018 Jijini Paris akiwa na miaka 85 kwa kufanya onyesho Jijini Milan kuonyesha Nguo zake za mwisho alizohusika kuzibuni kabla hajafariki.

Kupitia mwaka  1980  Karl Lagerfeld aliweza kurudisha kampuni ya Chanel kwenye soko baada ya kampuni hiyo kuyumba na kupoteza muelekeo na ndipo baadhi ya watu walipooanza kununua bidhaa kutoka kwenye kampuni hiyo ya Chanel.

Karl Lagerfeld alikuwa miongoni mwa watu ambao walikuwa nyuma ya pazia kwenye mafanikio ndani ya brands kama Tommy Hilfiger, Chanel na Fendi mwaka 1980. Onyesho hilo lilihusisha wanamitindo maarufu akiwemo Kaia Gerber, Bella Hadid, Gigi Hadid na wengine wengi.

MAPYA KESI YA WEMA: VIDEO YAKE YA NGONO YACHAMBULIWA MAHAKAMANI

Soma na hizi

Tupia Comments