Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

U HEARD: Mama Wema afungukia wanaomuuza Wema kwa Wanaume

on

November 4, 2016 U Heard ya XXL Clouds FM inayo sauti inayodaiwa ni ya Mama mzazi wa mwigizaji Wema Sepetu akilalamika kuhusu marafiki wa Wema kumtumia kwaajili ya kujinufaisha wao kibiashara kwa kumuuza kwa wanaume.

Mama Wema anasikika akisema kuna Rafiki wa mwanae anaitwa Muna alichukua nguo ya ndani ya Wema ili aipeleke kwa waganga kwaajili ya kuchukua nyota yake ambapo Wema alipotafutwa na Soudy Brown amejibu hana tatizo na Muna.

“Jamani hakuna kitu kama hicho, mi niko poa na Muna… Hebu niacheni jamani nina usingizi bwana, ila dah hilo jina la Muna (Ma****) kama limekick hivi haki ya Mungu daaah! Binadamu sio watu wa mchezo aisee: – Wema Sepetu

Hivi karibuni zilisambaa sauti zinazodaiwa ni za mama Wema zikisema kwamba marafiki wa Wema wanamtumia kibiashara huku Wema akilalamika kuwa Muna amekuwa amkimpa taarifa za uongo mama Wema ili aonekane mbaya.

“Yaani kwakweli Wema hatofika popote kuna wale marafiki zake ni wachonganishi wengine ni watu wazima sababu wengi wanamtumia kumuuza kwa wanaume na wakimkosa wanaanza kutunga mambo ambayo sio, na Wema anaweza kuambiwa kuna mtu anakuja kukuchoma mkuki, hata akiambiwa mama yako anakuroga anaweza kuja mbio na anayabeba kama yalivyo’ – Mama Wema Sepetu

Kupata full stori Bonyeza Play hapa chini kusikiliza.

VIDEO: Majibu ya Video Queen aliyeonekana kwenye Video ya Salome amejibu kuwa siyo yeye aliyebakwa. 

VIDEO: Uliikosa ya Wema Sepetu na sababu za kuwagombeza Team Wema? bonyeza play hapa chini kutazama

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement