Habari za Mastaa

Kusaga kasema Tigo Fiesta lazima ifanyike kabla mwaka haujaisha

on

Ikiwa leo December 4,2018 Kampuni ya Clouds Media Group (CMG) inatimiza miaka 19 tokea ianzishwe, Joseph Kusaga ambaye ni Mkurungezi mtendaji wa kampuni hiyo ametangaza kuhusu tamasha la Fiesta kufanyika kabla ya mwaka huu kuisha.

Tamasha la Fiesta jijini Dar Es Salaam lilitakiwa kufanyika November 24,2018 na mwisho wa siku liliahirishwa na kutofankyika huku sababu ya msingi haikutajwa zaidi ya Viongozi kusema kuwa tatizo hilo lilikua nje ya uwezo wao.

“TIGO FIESTA 2018 lazima ifanyike kabla mwaka kuisha,nimezungumza hadi na Mh Rais Dkt Magufuli kwamba pengine suala ni venue hili jambo limepenyezwa kwa viongozi wa serikali tumekaa tumezungumza” >>>Joseph Kusaga 

Mama wa Msanii wa BongoFleva aliyetambulishwa kuingia kwenye Bongomovie

Soma na hizi

Tupia Comments