Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Alichokiandika Alikiba baada ya kuonekana Wizkid alipewa tuzo MTV EMA kimakosa

on

November 9 2016 ndio siku ambayo taarifa za waandaaji wa tuzo za MTV EMA walimtumia taarifa Alikiba kupitia uongozi wake kuwa ni mshindi wa tuzo ya Best African Act na kuwa ilitolewa kwa Wizkid wa Nigeria kimakosa ila yeye ndio alistahili kuwa mshindi wa tuzo hiyo kwa mwaka 2016.

Siku moja baada ya MTV EMA kumfikishia taarifa hizo za ‘kumpokonya’ hiyo tuzo Wizkid, Alikiba ametumia ukurasa wake wa instagram kuwashukuru mashabiki wake, vyombo vya habari na wote wanaomuunga pamoja na waandaaji wa tuzo hizo.

“Namshukuru MUNGU Na Shukrani kwa MTV kwa heshima hii, nina furaha sana kwa ushindi huu, ni heshima kwangu na nchi yangu Tanzania ?? pamoja na East Africa nzima kiujumla. Shukrani sana kwa familia yangu, management yangu na mashabiki zangu wote – nawapenda sana#bloodfanswaalikiba #Kajiandae#KingKiba

VIDEO: Ipo hapa Exclusive kuhusu MTV EMA kuichukua tuzo ya BEST AFRICAN ACT kwa Wizkid na kumpa Alikiba 

VIDEO: Alikiba alivyotumbuiza kwenye FIESTA 2016 Dar es salaam, tazama hii video hapa chini

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement