PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Top Stories

Wema Sepetu afika Mahakamani baada ya kutoka India, Alichoamua Hakimu

on

Leo June 13, 2018 Msanii Wema Sepetu anayekabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya amefika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu katika kesi yake ikiwa ni wiki chache baada ya kuelezwa amekwenda nchini India kufanyiwa upasuaji.

Taarifa ya Wema kwenda nchini India kufanyiwa upasuaji ilitolewa na Mama yake mzazi baada ya upande wa mashtaka kuhoji kwanini hayupo mahakamani.

Katika kesi hiyo Wema na wenzake wanatetewa na wakili Albert Msando walifika mahakama hapo kwa ajili ya kuanza kujitetea lakini ilishindikana baada ya kesi hiyo kuahirishwa hadi June 19,2018.

Wakili wa serikali, Constantine Kakula alimueleza Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba kuwa kesi hiyo imeitishwa ili washtakiwa waanze kujitetea lakini wanaomba ahirisho kutokana na mawakili wa pande zote mbili kuwa na udhuru.

Baaada ya kusema hayo, Hakimu Simba alikubali hoja hiyo ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi June 19,2018 kwa ajili ya kuanza kujitetea.

Mbali na Wema, washtakiwa wengine ni Angelina Msigwa na Matrida Abbas.

Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kuzitumia.

Inadaiwa Februari 4, 2017 katika makazi ya Wema eneo la Kunduchi Ununio, washtakiwa walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.

Kwa upande wa Wema yeye anadaiwa kuwa February mosi 2017 katika eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam, alitumia dawa za kulevya aina ya bangi.

Mbowe na Viongozi CHADEMA wasomewa mashtaka mapya 13

Soma na hizi

Tupia Comments