Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Tayari zimepigwa mechi 6 za Premier League leo… matokeo ninayo

on

Ligi kuu ya England imeendelea leo October 14, 2017 ambapo mechi sita kati ya saba za leo tayari zimemalizika ambapo kwenye game ya mapema kabisa Liverpool ikiwa mwenyeji wa Manchester United katika uwanja wa Anfield, full time imekua ni 0-0.

Mechi nyingine ilikua ni ya Manchester City waliokuwa nyumbani vs Stoke City ambapo Man City waliibuka na ushindi wa mabao 7-2 yaliyofungwa na Jesus aliyefunga mawili, Sterling, Silva, Fernandinho, Sané na Bernardo Silva huku magoli ya Stoke yakifungwa na Diouf na bao la Walker aliyejifunga.

Wilfried Zaha alifunga goli la ushindi Crystal Palace ikiwafunga mabingwa watetezi Chelsea 2-1 na kupata ushindi wao wa kwanza wa Premier League msimu huu, Palace walikuwa wa kwanza kupata bao baada ya Azpilicueta kujifunga lakini Bakayoko alisawazisha kabla ya Zaha kufunga la ushindi.

Tottenham nayo ikapata ushindi wa 1-0 vs AFC Bournemouth huku goli pekee likifungwa na Christian Eriksen huku Burnley ikitoka sare ya 1-1 vs West Ham katika uwanja wa Turf Moor.

Swansea City imepata ushindi wa kwanza nyumbani kwenye Premier League msimu huu baada ya kuifunga Huddersfield Town mabao 2-0 katika uwanja wa Liberty.

ALL GOALS: Taifa Stars vs Malawi October 7 2017, Full Time 1-1

Soma na hizi

Tupia Comments