Premier Bet

Michezo

Pep Guardiola atangazwa kuwa kocha bora 2018/2019

on

Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Ligi ya England Man City Pep Guardiola ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya kocha bora wa msimu wa 2018/2019, Pep Guardiola katangazwa kuwa mshindi wa tuzo hiyo usiku huu wakati wa utoaji wa tuzo za waliofanya vizuri EPL 2018/2019.

Pep Guardiola ambaye ameiwezesha Man City kutetea Ubingwa wake wa EPL msimu huu, kipengele hicho alikuwa akichuana na makocha  wa Liverpool Jürgen Klopp, Tottenham Mauricio Pochettino na kocha wa Wolves Nuno Espírito Santo.

Man City wamefanikiwa kutwaa Ubingwa wa EPL kwa mara ya pili mfululizo, baada ya kufanikiwa kukusanya jumla ya poiny 198 ndani ya misimu miwili, chini ya Pep Guardiola (48) aliyewahi kuzifundisha club za FC Barcelona na FC Bayern Munich, Man City pia wanasubiri kucheza fainali ya FA May 18 2019 dhidi ya Watford.

Mzee Muchacho na Fahad wambananisha Haji Manara avae jezi ya Yanga SC

Soma na hizi

Tupia Comments