PremierBet Tanzania Usain Bonus Ad

Michezo

Ndani ya siku 120 Simba SC itaanza kumiliki uwanja wake

on

Hii inaweza kuwa moja kati ya habari kubwa kwa wapenzi wa soka Tanzania au mashabiki wa Simba iliyotolewa Jumatano ya October 3 2018 kupitia ukurasa rasmi wa muwekezaji ndani ya club ya Simba na mfanyabiashara Mohamed Dewji.

Mohamed Dewji leo ametangaza rasmi kuwa Simba SC hadi kufikia mwezi wa pili mwaka 2019, Simba SC itaanza kutumia uwanja wake wa Bunju kwa ajili ya mazoezi, kwa kauli hiyo ya MO Dewji maana yake ujenzi wa uwanja huo utakamilika mapenza zaidi.

Kwa mujibu wa kauli ya MO Dewji kupitia ukurasa wake wa instagram ni kuwa Simba itakuwa inatumia uwanja wake wa mazoezi ndani ya siku 120 kutokea sasa.

“Huu ni wakati wa kihistoria kwa klabu yetu. Kwa miaka mingi nimekuwa nikiota na sisi tuwe na uwanja wetu wa mazoezi, na ninafurahi sasa ninawezesha hii ndoto baada ya miaka 82 tangu kuanzishwa kwa klabu yetu ya #Simba.”

“Nimeanza kukamilisha ahadi ya uwanja wa Bunju. Insha’Allah kazi ya ujenzi itakamilika kabla ya mwezi wa 2, 2019. #NguvuMoja 🙏🏽”

“Simba tumewaachia, sisi hatuna presha”-Kocha wa Yanga

Soma na hizi

Tupia Comments