Juzi kulikua na baadhi ya msg zinatembea na wengine wakiandika kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mfululizo wa matukio yanayowapa Wananchi hofu kwenye mkoa wa Mwanza, kabla ya bomu lililosikika juzi kuna mauaji ya Watu 7 wa nyumba moja kwa kukatwa Mapanga yalitokea lakini pia Mwenyekiti wa mtaa kuuwawa kwa risasi na Watatu kuchinjwa ndani ya Msikitini.
Kuhusu bomu lililosikika juzi na kuzua hofu, Kamanda wa Polisi Mwanza Ahmed Msangi ameongea na millardayo.com na kusema yafuatayo >>> ‘Tulikua kwenye Oparesheni zetu tulikwenda kuwatimua watu na ile milipuko yenyewe ni sisi wenyewe tulipiga bomu la kishindo kwasababu kulikua na vijana wengi, hatukutaka walete vurugu‘
‘Sio Majambazi walipiga risasi ni uoga tu Wananchi… Mwanza iko salama.. ni matukio tu ya kawaida sana ambayo yanatokea kama sehemu nyingine, watu wanasema Mwanza sio salama sababu ya yale mauaji ya Sengerema ila kiukweli hali ya Mwanza ni shwari’ – Kamanda Msangi
‘Watu tu wanakuza mambo wanakuza taarifa….. mimi nawakaribisha hata wanaotaka kuja kufanya biashara waje… yeyote anaetaka kuja Mwanza aje, Mwanza iko salama‘
ULIIKOSA HII? KUTANA NA TRAFIKI MWENYE MBWEMBWE DAR ES SALAAM, FOLENI HAISIMAMI AKIWEPO…
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE