AyoTV

VIDEO: Tundu Lissu afunguka ishu ya kutaka kupimwa mkojo na mengine

on

Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa TLS Tundu Lissu amekutana na Waandishi wa Habari ikiwa ni saa chache tu baada ya kuachiwa kwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo 27, 2017 na kuzungumzia mambo mbalimbali ikiwepo ishu ya kutaka kupimwa mkojo.

>>>”…nikaingizwa kuna kuna nyumba karibu na Ocean Road nikaambiwa Mheshimiwa tunahitaji mkojo wako tuupime, nikawaambia nyie Askari mimi nimeshtakiwa kwa uchochezi, kupima mkojo kunathibitishaje uchochezi?” – Tundu Lissu.

Lissu ambaye anatetewa na Mawakili 18, wakiongozwa na Fatma Karume amepata dhamana kwa kutimiza masharti baada ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kutupilia mbali ombi la upande wa mashtaka la kumnyima dhamana.

VIDEO hii ina kila kitu alichoongea Tundu Lissu baada ya kuachiwa na Mahakama kwa dhamana…tazama kwa kubonyeza play!

ULIPITWA na hii VIDEO? Alichozungumza Wakili Fatma Karume baada ya Tundu Lissu kupewa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu…bonyeza PLAY kutazama!! 

Soma na hizi

Tupia Comments