Habari za Mastaa

#Exclusive Ni kweli Ali Choki na Nyamwela wamerudi Twanga Pepeta! maneno ya Asha Baraka je umeyapata?

on

drums 2Mpaka April hii ya 2015 kwenye muziki wa dance Tanzania hii haikosi kuwa kwenye stori 2 za juu nina uhakika, tunajua Ali Choki ndio alikua anaimiliki band ya Extra Bongo na baadae aliwachukua watu kama Banza Stone na Super Nyamwela lakini April 8 2015 headlines zimegeuka.

Mkurugenzi Asha Baraka ameongea kwenye Exclusive interview na Millard Ayo baada ya Ali Choki na dancer Super Nyamwela kutangazwa kurudi Twanga Pepeta >>> ‘Kwanza tulikua na kutokuelewana nafikiri ni kibiashara kati yangu mimi na Ali Choki lakini baadae watu wazima wakakaa wakaona ili kukuza tasnia wakatuweka chini Global Publishers na wakatuweka sawa

Choki Super

Ali Choki, Luiza na Super Nyamwela mbele ya vipaza sauti kutangaza haya maamuzi mapya, picha ilipigwa na sufianimafoto.com

‘Kilichotokea baada ya hapo Ali Choki alikwenda Japan kwenye safari zake na akiwa huko akasikia huku nyumbani Wanamuziki wake wametawanyika naona akaona ni vigumu tena kuanzisha Band na kujipanga upya kwa hiyo akaamua kurudi kwenye Band yake ya Twanga Pepeta iliyomkuza na kumfanya kuwa Choki’ – Asha Baraka.

Unataka kuyasikia mengine aliyoyasema Asha Baraka? bonyeza play hapa chini…

millardayo.com ndio sehemu yako kuzipata story zote mtu wangu, unaweza kuwa karibu zaidi na mimi kwa kujiunga kwenye Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments