Stori Kubwa

Muonekano wa gari la Mwamvita Makamba baada ya kurushiwa mawe na risasi South Africa.

on

image-20-04-15-08-47-1Mwamvita Makamba ni mtoto wa Mzee Yusuf Makamba na ni dada wa Naibu Waziri January Makamba ambaye amekua akitajwa kwa uzito kwenye headlines za uchaguzi mkuu wa Tanzania 2015.

Stori kwenye headlines hivi karibuni Mwamvita aliandikwa na baadhi ya magazeti kwamba baada ya January kutajwa kwenye headlines za uchaguzi mkuu, Mwamvita avamiwa na watu wenye silaha Johannesburg Afrika Kusini.
image-20-04-15-08-47Baada ya hizo headlines kuendelea Mwamvita anaefanya kazi na kuishi Afrika Kusini alikubali kuongea kwenye Exclusive interview na millardayo.com na kusema >>> ‘Hii haihusiani na January kugombea Urais na wala haihusiani na uvamizi unaofanywa kwa wageni Afrika Kusini, ilikua ni ajali tu imenikuta nikisafiri kutoka Johannesburg kwenda Sun city jioni’

>>> ‘Nilipita eneo ambalo mchana Polisi walituambia kulikua na maandamano kwahiyo jioni ile walikua wamebakia wahuniwahuni wachache lakini sisi hatukuona sababu ilikua usiku, wakati tunapita mbele yetu ndio tukaona vijana wamechoma matairi’

>>> ‘Lilikua ni tukio la dakika 5 tu lakini ilikua hatari sana sababu wale vijana wengine walikua wameshafika kwenye kioo changu pembeni yani walikua wameshalizunguka gari, tunamshukuru Mungu tuko salama na hakuna aliyejeruhiwa’ – Mwamvita Makamba.

Unaweza kumsikiliza Mwamvita kwa kubonyeza play hapa chini..

 

Soma na hizi

Tupia Comments