Mgomo wa Madereva ulimalizwa mchana wa May 5 2015 kwenye stand kuu ya Ubungo muda mfupi baada ya Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda pamoja na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kuwasili.
Baada ya hapo kwanza kulikua na taarifa kwenye mitandao mbalimbali kwamba Paul Makonda hakuhusika kumaliza mgogoro huo bali Mwenyekiti Freeman Mbowe.
Kwenye Interview na millardayo.com Mwenyekiti Freeman Mbowe ameyasema yafuatayo >>> ‘Swala la mgomo wa madereva limekua na athari nyingi na tofauti kwa taifa na tangu mgomo umeanza jana watu mbalimbali wameathirika na upande wa pili bado ni ukweli tu kwamba hata madereva madai yao yana msingi na yanastahili kutatuliwa, kamati kuu ilinishauri nikaweze kuona naweza kuwa wa msaada gani’
‘Aliyefanya mazungumzo hasa rasmi na Madereva alikua ni mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda na nilipofika nilimkuta akiwa kwenye mazungumzo na viongozi wa madereva na kimsingi walikua walishaafikiana, nilichojaribu kukizungumza ni kuunga tu mkono kwasababu sikuona jambo baya lililofanyika na kuwatia moyo kwa upande huo’
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda atakutana na Waandishi asubuhi ya May 6 2015 kuzungumza yote yaliyoafikiwa baada ya kukutana na Waziri mkuu lakini kama ulimis alichokisema baada ya kumaliza mgomo, unaweza kumsikiliza hapa chini.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.