Michezo ya mwisho ya hatua ya Makundi ya Kombe la Mapinduzi kwa Kundi B imechezwa leo January 7 2017 katika uwanja wa Amaan Zanzibar, mchezo kati ya Yanga dhidi ya Azam FC ndio mchezo uliyokuwa unasubiriwa kwa hamu zaidi visiwani Zanzibar licha ya kuwa timu zote zilikuwa zimefuzu.
Katika mchezo huo Azam FC ambao wanaonekana walikuwa wanasuasua katika michuano hiyo, imewashangaza wengi kwa kuwafunga Yanga kwa goli 4-0, hiki ni kipigo cha pili kikubwa kwa Yanga kufungwa toka May 6 2012 alipofungwa goli 5-0 na Simba katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Magoli ya Azam FC yalifungwa na nahodha wao John Bocco dakika ya 2, Yahaya Mohamed dakika ya 54, Joseph Mahundi dakika ya 80 na goli la mwisho lilifungwa na Enock Atta aliyeingia akitokea benchi, Azam FC sasa atakuwa anaongoza Kundi B kwa kuwa na point 7 akifuatiwa na Yanga huku Zimamoto na Jamhuri zikiaga michuano hiyo.
ALL GOALS: JKT Ruvu vs Yanga December 17 2016, Full Time 0-3