Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameshuhudia utiaji saini wa mkataba wa mauziano ya mahindi kati ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) na Shirika la Chakula Duniani (WFP) uliofanyika Ikulu Jijini DSM.
Mkataba huo umetiwa saini na Kaimu Mtendaji Mkuu wa NFRA Vumilia Zikankuba na Mwakilishi na Mkurugenzi Mkazi wa WFP hapa nchini Michael Danford, ambapo WFP itanunua tani 36,000 zenye thamani ya shilingi Bilioni 21 kutoka NFRA.
Rais Magufuli ameitaka NFRA kujipanga vizuri katika shughuli zake ili kuondokana na utaratibu wa kuwa inapatiwa fedha kutoka Serikalini kila mwaka kwa ajili ya kununua mazao ya hifadhi ya chakula, ilihali mazao yaliyopo hifadhini yakiuzwa kiujanjaujanja kwa wafanyabiashara tena kwa bei ya kutupa.
“Nyinyi NFRA wapeni hawa WFP tani zote 45,000 wanazozihitaji, na hata wakihitaji tani 100,000 wapeni au hata 200,000 wapeni, mkipata hizo fedha nendeni mkanunue mazao ya wakulima wanaohangaika na soko. Lakini pia punguzeni matumizi makubwa ya fedha za kugharamia zoezi la ununuzi wa mazao” Rais Magufuli
IKULU LEO JPM “TUMBUENI HAO MCHWA WENGINE NILETEENI HATA LEO”