Mchezaji wa kimataifa wa Argentina anayeichezea klabu ya FC Barcelona ya Hispania Lionel Messi na baba yake mzazi Jorge Messi wanatuhumiwa kwa kosa la ukwepaji kodi na leo May 31 2016 inaripotiwa kesi yao kuanza kusikilizwa katika jiji la Barcelona Hispania.
Messi ambaye ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia mara tano, anajiandaa na michuano ya Copa America itakayofanyika mwaka huu USA, lakini kesi inayomkabili ya ukwepaji kodi wa Pound milioni 3.2 ambazo ni zaidi ya bilioni 10 za kitanzania imeanza kusikilizwa.
Kiasi cha kodi wanachodaiwa Messi na baba yake, walikwepa kulipa kodi hiyo kati ya mwaka 2007 na 2009 wakati mauzo ya picha za staa huyo wa FC Barcelona, ofisi ya waendesha mashtaka wamependekeza Lionel Messi na baba yake wahukumiwe miezi 22 jela.
ALL GOALS: Azam FC Vs Esperance ya Tunisia April 10 2016 (Full Time 2-1)
https://youtu.be/duzv5kA8Q-c
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE